TAAS MKOANI KATAVI WAMEKATAA KUITWA WALEMAVU WA NGOZI
Na.Issack Gerald Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAAS) Mkoani Katavi kimewataka watanzania kutowaita wao kama watu wenye ulemavu wa ngozi albino badala yake wawaite watu wenye Ualbino. Mwenyekiti wa TAAS Mkoani Katavi Victus Kweka Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Katavi Bw.Victus Kweka kupitia kikao cha kujadili kupinga ukatiri,unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za w atu wenye ulemavu kwa kuwanyima haki za msingi kama elimu,afya na haki nyingine za kibinadamu. Amesema rangi ya ngozi waliyonayo watu wenye ualbino siyo ulemavu wa ngozi bali wao wanahesabika katika kundi la watu wenye ulemavu wa macho kutokana hali waliyonayo. Kwa upande wake mratibu wa wa elimu jumuishi Wilayani Mpanda Bi.Ashura Shabaani ambaye pia ni msichana mwenye ualbino amesema mpaka sasa bado kuna baadhi ya watu wenye ualbino wanaojinyanyapaa. Amewataka watu wenye ualbino kuchanganyikana na jamii ili kupata elimu inayowawezesha kufahamu haki zao,kupatiwa mafuta ya kupu...