Posts

Showing posts from November 30, 2017

WAJUMBE CCM KATAVI:UCHAGUZI ULIKUWA NA DOSARI

Image
Na.Issack Gerald Baadhi ya wajumbe wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi wamedai uchaguzi wa ndani kupitia jumuia za chama hicho kuwa na dosari. Katibu wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi Kajoro Vyohoroka ambaye  ameeleza zoezi hilo kufanyika  vizuri huku akiongeza kusema kuwa anafuatilia katika jumuia zote ili kujua kama kulikua na changamoto zilizojitokeza. Uchaguzi wa kupata viongozi mbalimbali wa jumuia za chama cha Mapinduzi ulifanyika jana. Uchaguzi kama huo ndani ya chama cha Mpainduzi,umefanyika pia Zanzibar. Habari Zaidi NA P5TANZANIA LIMITED

LEO NI MAADHIMISHO SIKU YA MAULIDI

Image
Na.Issack Gerald Waisilamu wilayani Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla wameombwa kuhudhuria maulidi ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Mtume Mohamadi yanayofanyika leo. Wito huo umetolewa na Shehe wa baraza kuu la waisilamu Tanzania BAKWATA Wilaya ya Mpanda  Iddi Shabani Kondo Wakati akizungumza na Mpanda Redio ambapo amewaomba waisilamu wote kudumisha amani kataika hadhara hiyo . Shehe Kondo amesema kuwa Maulidi hiyo itafanyika katika kata ya Stalike halmashauri ya nsimbo kuanzia saa 1:30 jioni. Amesema katika kuadhimisha siku hiyo waisilamu wote wanakumbuka kazi iliyofanywa na mtume Mohamadi ya kufikisha ujumbe rasmi wa mafundisho wa uisilamu. Maulidi hii ya mwaka 1439 wa dini ya kiisilamu sawa na mwaka 2017 kitaifa yatasomwa wilayani Ruangwa Mkoani Lindi na tarehe 1/12 itakuwa ndio siku ya mapumziko. Habari Zaidi NA P5TANZANIA LIMITED

HALI YA TAHARUKI MKOANI RUKWA,JENEZA LENYE MWILI WA MAREHEMU LIMETELEKEZWA

Image
Na.Issack Gerald Hali ya taharuki na hofu imezuka katika Kijiji cha Katani Kata ya Nkandasi wilayani Nkasi mkoani Rukwa na kusababisha waombolezaji kutimua mbio na kuacha jeneza lenye mwili wa marehemu baada ya mvua kubwa kuanza kunyesha na kubomoa nyumba za wakazi wa kijiji hicho. Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kaungo, Robert Kanoni, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 6 mchana,  wakiwa wanaelekea kufanya maziko ya marehemu Dismas Kanoni aliyefariki jana baada ya kuugua siku chache zilizopita, ghafla ilianza kunyesha mvua kubwa ikiambatana na radi na upepo mkali ulioezua baadhi ya nyumba hali iliyosababisha baadhi ya waombolezaji kutimua mbio na kurejea majumbani kutokana na hofu iliyoibuka kufuatia tukio hilo. Baadhi ya wananchi walivumilia nakurejea na jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu nyumbani na kuahirisha maziko kwa muda ili kupisha hali hiyo itulie na walikwenda kuzika baadaye katika makaburi yaliyopo kijijini hapo. Alisema tukio hilo limezua hisia ...

WAKAZI MPANDA WANAISHI KWA HOFU YA USALAMA, WASHINDWA KUFANYA KAZI

Image
Na.Issack Gerald Wakazi wa vijiji vya Ndui Stesheni,Mnyaki A na Mnyaki B kata ya Katumba wilayani Mpanda Mkoani Katavi wanashindwa kufanya kazi za maendeleo kwa uhuru kutokana na uharifu unaofanywa na watu wasiojulikana. Hali hiyo imebainishwa na wakazi wa vijiji hivyo wakati wakizungumza na Mpanda Radio kwa Nyakati tofauti katika vijiji hivyo kutokana na matukio ya watu kuvamiwa nyumbani nyakati za usiku,kutekwa njiani na kuporwa mali. Wakazi wameliomba jeshi la polisi kuweka mkazo ili kutafuta namna ya kukomesha uharifu huo ambao umekuwa kero kwao. Mmoja wa viongozi katika maeneo hayo Bw.Hussein Nasri ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ndui Stesheni,amekiri kuwepo kwa matukio ya kiuharifu hasa unyang’anyi wa pikipiki matukio ambayo hivi karibuni yameripotiwa na wenyeviti wa vijiji vya Mnyaki A na Mnyaki B. Hivi karibuni,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda,akihojiwa na Mpanda Radio,alitoa kauli kuwa hajapokea za taarifa za kiuharifu za hivi karibuni hali ambay...