SIKU 11 ZA VIKAO VYA BUNGE KUANZA KESHO JANUARI 30,2018
Bunge la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kuanza mkutano wa 10 wa Bunge hilo kuanzia kesho Januari 30. Kwa mjibu wa taarifa ya bunge ambayo imetolewa leo na kitengo cha habari,elimu na mawasiliano kutoka Ofisi ya Bunge inaeleza kuwa miongoni mwa shghuli za kesho ni pamoja na kiapo cha uaminifu kwa wabunge wateule watatu ambao ni Mh.Dkt.Damas Daniel Ndumbaro mbunge wa Songea Mjini,Mh.Monko Justine Joseph mbunge wa Singida Kaskazini na Mh.Dkt.Stephano Lemomo Kiruswa. Aidha kwa mjibu wa taarifa hiyo kutakuwa na kipindi cha maswali na majibu,miswada ya serikali pamoja na taarifa za kamati za kudumu za bunge. Vikao hivyo vinavyoatarajia kuanza kesho vinatarajia kufikia tamati Februari 9 mwaka huu. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED