MARUFUKU VITUO VYA POLISI KUCHOMWA MOTO
JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limekaririwa likisema linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kuchoma kituo kidogo cha Polisi kilichopo Mofu wilayani Kilombero baada ya kukivamia kwa lengo la kutaka polisi wawape mtuhumiwa wa mauaji ili wamuue. IGP ERNEST MANGU Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alibainisha kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 20, mwaka huu na chanzo ni wanakijiji wapatao 100 kufika katika kituo hicho wakimtaka mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe. Tukio la kuchomwa kwa kituo hicho limetokea ikiwa ni siku chache baada ya wananchi wenye hasira kuvamia Kituo cha Polisi Bunju A kilichopo Dar es Salaam na kukichoma moto kwa kile kilichoelezwa ni dereva kumgonga mwanafunzi na kupoteza maisha. Tuseme tu hapa kuwa utamaduni huu wa kuchoma vituo vya Polisi ni lazima ukomeshwe kwa sababu si suluhu la wananchi kupata kile wanachodai zaidi ya kuisababishia Serikali hasara na wakati huo huo kukwamisha huduma nyingine za kijamii. Kama kuna tatizo limetokea ni...