Posts

Showing posts from August 28, 2015

CHADEMA WAPINGA TAMKO LA POLISI VIKUNDI VYA ULINZI NDANI YA VYAMA VYA SIASA ,CCM WAKUBALI

Na.Issack Gerald-MPANDA Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kimepinga kauli ya jeshi la Polisi Mkoani hapa kupiga marufuku vikundi vya ulinzi katika vyama vya siasa wakati wa kampeni na uchaguzi.

CWT MPANDA YAKANUSHA KUWEPO MGOMO WA WALIMU JUMATATU AGOSTI 30

Na.Issack Gerald- MPANDA CHAMA  cha Walimu CWT Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Kimekanusha taarifa za Kuwepo kwa Mgomo wa Walimu siku ya Jumatatu wa Kuishinikiza serikali kuwalipa  Madai yao. Akingumza jana na P5 TANZANIA Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Mpanda bwana Jumanne Msomba amesema Ofisi yake haina taarifa za Mgomo huo na kuwataka walimu kusubiri tamko la Rais wa Chama cha Walimu taifa. Wakati   taarifa za kuwepo kwa  Mgomo wa walimu Wilayani Mpanda zikikanushwa  Kesho  Viongozi wa Chama cha Walimu taifa wanatarajia Kukutana na Viongozi wa Serikali ili kutafuta suluhisho la Madai hayo.

WANAFUNZI WAOMBA KUENDELEZWA ELIMU

Image
Wanafunzi wakiwa darasani Shule ya msini Mpanda iliyopo Manispaa ya Mpanda NA.Issack Gerald-Mpanda Wanafunzi wa shule ya msingi Mpanda  iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamewaomba wazazi na walezi kuwaendeleza kielimu wanapokuwa wamehitimu masomo ya darasa la saba na kufaulu kujiunga na kidato cha kwanza.

VIKUNDI VYA ULINZI VYAMA VYA SIASA VYAPIGWA MARUFUKU

Na.Issack Gerald-KATAVI Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limevitaka vyama vya siasa na wafuasi wao kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za vyama vyao kudumisha amani ya nchi na kuepuka makosa ya jinai yanayoweza kuwatia hatiani.

SIDO KUFUNGUA OFISI ZAKE KATAVI

Na.Issack Gerald-KATAVI Shirika la viwanda vidogovidogo SIDO Mikoa ya Ruka na Katavi, linatarajia kuanzisha ofisi Mkoani Katavi kusogeza huduma na kutatua changampoto mbalimbali   zinazowakabili wafanyabiashara zikiwemo mikopo na masoko