MKUU WA WILAYA YA MPANDA AINGILIA KATI MGOGORO WA TENDA YA WAJASILIAMALI KUHUSU UTENGENEZAJI WA MADAWATI.
Na.Issack Gerald-Katavi Umoja wa wajasiliamali Pasifiki waliopo mtaa wa majengo kata ya Kashaulili umeilalamikia Manispaa ya Mpanda kwa kutoa tenda kwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Sailoni Mwagama ambaye ni mjasiliamali wa eneo hilo tofauti na ilivyokuwa awali kuwa wajasiliamali hao wangepata tenda hiyo kwa pamoja kama ilivyokuwa imetangazwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw.Pazza Mwamlima.