SERIKALI YA MKOA WA KATAVI YAKATAA WAKANDARASI WASIOFUATA MASHARTI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI.
Na.Issack Gerald-Katavi
SERIKALI
Mkoni Katavi imesema haitakubali Kuingia Mikataba ya Ujenzi wa Miradi
mbalimbali ikiwemo barabara na wakandarasi wanaoshindwa Kufuata Masharti ya Utekelezaji wa Miradi hiyo.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahim Msengi wakati akizungumza na wajumbe wa bodi ya barabara ya Mkoa mkoani
Katavi Katika Kikao cha bodi hiyo kinacholenga Kujadili changamoto za
Miundombinu na jinsi ya Kuzitatua.
Katiki
Kikao hicho Wajumbe wametoa pendekezo la Kuundwa kwa Kamati itakayofuatilia
Ujenzi wa daraja la Mto koga linalounganisha Mikoa ya Katavi na Tabora Kufuatia
kuharibiwa na Mvua zinazoendelea Kunyesha na Kusababisha Kukosekana kwa Mawasiliano
ya Miundo Mbinu baina ya Mikoa hiyo.
Katika
daraja la mto Koga,watu 10 walipoteza maisha baada ya gari walilokuwa
wakisafiria wakati wakitoka Mkoani Tabora kuingia Mkoani Katavi.
Kwa
upande wake Mbunge wa jimbo la Kavuu Bi.Pudensiana Kikwembe,ameshauri kuepuka
gharama za ulipaji wa fidia zisizokuwa za msingi.
Comments