STENDI MPYA YA MABASI MPANDA KUANZA KUTUMIKA MWANZONI MWA 2018
Na.Issack Gerald Mstahiki Meya wa M anispaa ya Mpanda mkoani katavi Willium Mbogo amesema stendi kuu ya mabasi ya kisasa inatarajiwa kuanza kufanya kazi mwanzoni wa mwaka 2018. Mh.Mbogo amesema hatua iliyobaki ni ujenzi wa vibanda na kukamilisha huduma ya maji na umeme. Aidha amesema stendi hiyo itakuwa na uwezo wa kuingiza mabasi 60 kwa wakati mmoja ambapo ametoa wito kwa wamiliki wote wa mabasi kununua mabasi yanayoenda na hadhi ya stendi. Mkoa wa Katavi umefikisha miaka mitano toka kuanzishwa kwake huku ukipiga hatua kubwa ya kimaendeleo ukilinganisha na mikoa mingine michanga. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED