STENDI MPYA YA MABASI MPANDA KUANZA KUTUMIKA MWANZONI MWA 2018


Na.Issack Gerald

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda mkoani katavi Willium Mbogo amesema stendi kuu ya mabasi ya kisasa inatarajiwa kuanza kufanya kazi mwanzoni wa mwaka 2018.

Mh.Mbogo amesema hatua iliyobaki ni ujenzi wa vibanda na kukamilisha huduma ya maji na umeme.

Aidha amesema stendi hiyo itakuwa na uwezo wa kuingiza mabasi 60 kwa wakati mmoja  ambapo ametoa wito kwa wamiliki wote wa mabasi kununua mabasi yanayoenda na hadhi ya stendi.

Mkoa wa Katavi umefikisha miaka mitano toka kuanzishwa kwake huku ukipiga hatua kubwa ya kimaendeleo ukilinganisha na mikoa mingine michanga.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA