Posts

Showing posts from October 21, 2017

SHIRIKA LA WATERLEED WAMETOA MSAADA WA GARI 1 NA PIKIPIKI 26 KATIKA MKOA WA KATAVI

Image
Na.Issack Gerald-Katavi Shirika la Waterleeds  Program  Tanzani  WRP-T limetoa msaada wa  gari moja kwa  Manispaa ya  Mpanda na pikipiki 26 kwa Halmashauri za mkoa wa  Katavi zenye thamani ya  zaidi ya shilingi milioni 268.

RAIS MGABE AMETEULIWA NA UN KUWA BALOZI MWEMA WA AFYA

Image
Shirika la afya duniani WHO limemteuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kama 'balozi mwema ' katika kusaidia kukabiliana na magonjwa yaliyosahaulika . Akifafanua uamuzi wa uteuzi huo,Mkurugenzi mkuu mpya wa W.H.O.Dr Tedros Adha-nom Ghebre-yesus,alisifu namna Zimbabwe inavyozingatia afya ya umma. Lakini wakosoaji wamesema katika kipindi cha miaka thelathini na saba ya utawala wa rais Mugabe,huduma za afya zimekuwa mbaya ambapo wahudumu wa afya wamekuwa hawalipwi mara kwa mara na kumekuwa na ukosefu mkubwa wa dawa muhimu . Dr.Tedros ni raia wa Ethiopia ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza shirika la W.H.O. na alichaguliwa kwa ajili ya kukabiliana na kile kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo kuwa la kisiasa.

AJALI YA NDEGE CHINI KENYA

Ndege moja aina ya helikopta imeanguka katika ziwa Nakuru nchini Kenya muda mfupi baada ya kuondoka katika hoteli moja mjini humo.

WALIOUAWA KWA BOMU SOMALIA IMEFIKIA 358

Image
Mlipuko wa bomu Somalia uliowauawa zaidi ya watu 350 Serikali ya Somalia imesema idadi ya watu waliokufa katika shambulio kubwa la bomu la ndani ya Lori katika mji mkuu Mogadishu Jumamosi iliyopita imeongezeka na kufikia hadi watu 358. Lori lililipuka katika barabara ya makutano yenye shughuli nyingi na kuharibu hoteli,ofisi za serikali na migahawa . Hata hivyo haijabainika ikiwa eneo hilo la makutano ndilo lililolengwa au dereva wa Lori alilipua vilipuzi kwa sababu tayari watu walikuwa wameanza kushuku lori lake . Maafisa wamelilaumu kundi la wanamgambo wa al-Shabaab kwa shambulio hilo,lakini kundi hilo bado halijasema kuwa lilihusika na mlipuko huo Mlipuko huo uliwajeruhi watu zaidi ya mia mbili

MIKOA NA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI MATOKEO DARASA LA SABA 2017

Image
Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza  matokeo ya mtihani  wa darasa la saba huku Mkoa wa Katavi ukiwa ni miongoni mwa mikoa kumi bora ambayo imefanya vizuri kwa kufaulisha wanafunzi.

AJALI YA MOTO IMEUA WATU 4 USIKU WA KUAMKIA LEO

Image
Watu wanne wamepoteza maisha usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha fumba wilaya ya Magharibi B Unguja kutokana na nyumba kuteketea kwa moto mnamo majira ya saa sita na nusu usiku.