WALIOUAWA KWA BOMU SOMALIA IMEFIKIA 358
Mlipuko wa bomu Somalia uliowauawa zaidi ya watu 350 |
Serikali ya Somalia imesema idadi ya
watu waliokufa katika shambulio kubwa la bomu la ndani ya Lori katika mji mkuu
Mogadishu Jumamosi iliyopita imeongezeka na kufikia hadi watu 358.
Lori
lililipuka katika barabara ya makutano yenye shughuli nyingi na kuharibu
hoteli,ofisi za serikali na migahawa .
Hata hivyo
haijabainika ikiwa eneo hilo la makutano ndilo lililolengwa au dereva wa Lori
alilipua vilipuzi kwa sababu tayari watu walikuwa wameanza kushuku lori lake .
Maafisa
wamelilaumu kundi la wanamgambo wa al-Shabaab kwa shambulio hilo,lakini kundi
hilo bado halijasema kuwa lilihusika na mlipuko huo
Mlipuko
huo uliwajeruhi watu zaidi ya mia mbili
Comments