AJALI YA NDEGE CHINI KENYA
Afisa mkuu
wa Polisi mjini Nakuru Joshua Omukata amethibitisha kisa hicho akisema walikuwa
wakisubiri boti kufanya operesheni ya kuwanusuru waliokuwa wakiabiri ndege
hiyo.
Ripoti
zinasema kuwa kulikuwa na watu watano katika ndege hiyo ambapo Seneta wa Nakuru
Susan Kihika amesema watatu kati ya wale waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikuwa
wanachama wa kitengo chake cha mawasiliano.
Ndege hiyo iliondoka katika
hoteli ya Jarika County Lodge na taarifa zinasema ilikuwa ikipaa chini chini
kabla ya kuanguka ambapo Ndge hiyo ilitarajiwa kusafrisha waandishi wa habari
katika mkutano wa kampeni .
Waokoaji walikuwa bado
hawajaanza operesheni saa nne baada ya ndege hiyo kuanguka katika ziwa hilo kwa
ukosefu wa boti.
Waokoaji
walilazimika kusubiri boti kusafirishwa kutoka Ziwa Naivasha huku Mkurugenzi wa
Idara ya kitaifa ya kukabiliana na majanga Pius Masai akisema ndege ya polisi
imetumwa katika eneo hilo kusaidia katika uokoaji.
Comments