RAIS MGABE AMETEULIWA NA UN KUWA BALOZI MWEMA WA AFYA
Akifafanua
uamuzi wa uteuzi huo,Mkurugenzi mkuu mpya wa W.H.O.Dr Tedros Adha-nom
Ghebre-yesus,alisifu namna Zimbabwe inavyozingatia afya ya umma.
Lakini
wakosoaji wamesema katika kipindi cha miaka thelathini na saba ya utawala wa
rais Mugabe,huduma za afya zimekuwa mbaya ambapo wahudumu wa afya wamekuwa
hawalipwi mara kwa mara na kumekuwa na ukosefu mkubwa wa dawa muhimu .
Dr.Tedros ni raia wa Ethiopia ambaye ni Mwafrika
wa kwanza kuongoza shirika la W.H.O. na alichaguliwa kwa ajili ya kukabiliana
na kile kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo kuwa la kisiasa.
Comments