WAVUVI RUKWA WAIPONGEZA ZAMBIA KUONDOA ZUIO BIASHARA YA SAMAKI
WAVUVI wa samaki katika ziwa Tanganyika wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameishukuru serikali ya Zambia kwa kuondoa marufuku ya biashara ya samaki katika nchi hiyo. Marufuku hiyo ilikuwa imewekwa kwa takribani wiki mbili zilizopita kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu nchini humo.