RAIS MAGUFULI AFYANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA ULINZI WA ISRAEL IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel Mhe.Avigdor Lieberman Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.Hussein Ali Mwinyi,Balozi wa Israel hapa nchini Mhe.Noah Gal Gendler,viongozi wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi.

Kwa mjibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,Ikulu Gerson Msigwa,Katika mazungumzo hayo Mhe.Rais Magufuli amemshukuru Mhe.Lieberman kwa kuitembelea Tanzania na amemhakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ina dhamira ya dhati ya kuukuza zaidi na kuuimarisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Israel.
Mhe.Rais Magufuli ametaka makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Israel katika maeneo mbalimbali yakiwemo ulinzi na usalama,mafunzo na masuala ya kiuchumi yatiwe saini haraka ili utekelezaji uanze mara moja.
Aidha,Mhe.Rais Magufuli amemuomba Mhe.Lieberman kumfikishia ujumbe Waziri Mkuu wa Israel Mhe.Benjamin Netanyahu wa kumualika kutembelea Tanzania na pia kuanzisha ofisi ya ubalozi hapa nchini badala ya kutumia ofisi za ubalozi zilizopo Nairobi nchini Kenya.
Kwa upande wake Mhe.Avigdor Lieberman amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kumkaribisha na kufanya naye mazungumzo na pia amemhakikishia kuwa Israel imejipanga kuongeza uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania katika maeneo yote ya makubaliano pamoja na kusaidia kilimo na usindikaji wa chakula.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA