MKAZI MMOJA NSIMBO KATAVI AMEJINYONGA KWA KUTUMIA MKANDA WA SURUALI IKIELEZWA ANAKIMBIA MADENI
Na.Issack Gerald-Nsimbo Katavi Aliyekuwa Afisa Mtendaji katika kata ya Litapunga halmashauri ya Wilaya ya nsimbo mkoani Katavi Augastino Wangabo(52) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kile kilichoelezwa kuwa amekimbia madeni. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Smith Pangani amethibitisha mtumishi wake kujinyonga akisema tukio hilo limetokea jana. Amesema Marehemu Wangabo inasemekana alikuwa na madeni mengi pamoja na kutuhumiwa kula michango mbalimbali ikiwemo fedha ya maandalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru miaka ya hivi karibuni hali iliyopelekea kuondolewa katika kituo cha awali cha kazi alichokuwa amepangiwa na kurejeshwa Ofisini makao Makuu ya Halmashauri. Kwa upande wake kamanda wa polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amethibitisha marehemu kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali ambapo amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha marehemu kujinyonga. Kamanda Nyanda amesema mara baada ya marehemu kufuatwa nyumbani kwake kwa ajili...