HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA KUNUNUA GARI LA KUZOA TAKA,WAMESUBIRI KUBALI CHA WAZIRI MKUU
Na.Issack Gerald
Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani katavi Michael Nzungu amesema wamedhamiria kununua gari kwa ajili ya uzoaji taka wanachosubiri ni kibali kutoka kwa ofisi ya waziri mkuu.
Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu |
Amesema kwa sasa wanakodi gari ambalo bado halikidhi mahitaji ya mkoa hivyo wameanza kujihada za kununua gari ambalo mwaka huu litakuwa limeanza kazi.
Aidha amewataka wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi kifupi kilichobaki ili watatue kero ya kuzagaa kwa taka kwani gari dogo la manispaa linalotumika kwa sasa halitoshi kubeba taka zote .
Wananchi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mpanda wakiwemo waliopo katika kata za Mpanda Hoteli na Makanyagio wamekuwa wakilalamikia gari kutokuzoa taka hali inayosababisha mrundiano wa taka katika makazi ya watu na watu kuhofia kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu hasa msimu wa masika.
Hata Mkurugenzi Michael Nzyungu amewataka wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapoona taka zimerundikana ili utaratibu wa kuziondoa ufanyike.
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda yenye jumla ya kata 15 ilikuwa na magari mawili ya kuzoa taka lakini gari moja lililobaki halitosherezi kuzoa taka huku kila siku tani kadhaa za taka zikizalishwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments