KIJIJI CHA MAJALILA SASA MAKAO MAKUU RASMI YA HALMASHAURI YA WILAYA MPYA YA TANGANYIKA
Na.Issack Gerald
Bathromeo-Tanganyika
Kijiji cha Majalila kilichopo kata ya
Tongwe Halmshauri Mpya ya Tanganyika Mkoani Katavi, kimetangazwa Rasmi kuwa
Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Taarifa ya kijiji hicho kutangazwa
kuwa makao makuu ya Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika imetolewa jana na Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga wakati akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake.
Amesema kuwa ametangaza ili kumaliza
mvutano uliokuwepo kwa muda mrefu kwa serikali ya Halmshauri ya
Tangaznyika(Zamani ikiitwa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda) ili kuondoa mvutano uliokuwepo
hususani miongoni mwa madiwani ambao ni miongoni mwa viongozi wenye nguvu
katika Halmshauri kupanga masuala mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo.
Jenerali Muhuga amesema vijiji hatua
ya kutangazwa kijiji cha Majalila ni baada kikao cha kamati ya ushauri ngazi ya Wilaya iliyojadiliwa na madiwani
ambapo vijiji vilivyokuwa katika mchakato wa kuchaguliwa kuwa makao Makuu ya
Halmshauri ya Wilaya ni Majalila,Kamikusu na Migengebe.
Amesema kila kijiji kilitakiwa kiwe
na vigezo 11 ambavyo ni pamoja na
uarahisi wa eneo hilo kufikika,upatikana ji wa huduma za kijamii,uwepo wa
miundombinu za uhakika kama vile maji,barabara na mawasiliano,kuzingatia
uhifadhi wa mazingira,ulinzi na usalama wa eneo hilo na mtawanyiko wa wakazi
katika eneo hilo.
Wilaya ya Tanganyika ilitangazwa
rasmi na serikali Feberuari 4,2016 kwa
tangazo la serikali namba 68 ambapo wilaya hii inaundwa na tarafa 3,kata 16
pamoja na vijiji 55 ambapo mchakato ulipamba moto rasmi mwaka 2014 lakini kabla
ya mchakato wa awali kuanzawaka 2004.
Kijiji cha Majalila kimeonekana kuwa
na sifa nyingi kuliko vijjiji vya Kamikusu
na Migengebe.
SIFA YA KIJIJI CHA MGENGEBE
-Kipo km 78
kutoka Mpanda Mjini
-Eneo hili lipo
karibu na ushoroba wa hifadhi za wanayama kutoka hifadhi ya Katavi kwenda
hifadhi ya mahale Kigoma.
-Si rahisi
kufikika
-Lipo katika
chanzo cha maji Katuma hivyo uharibifu wa vyanzo vya maji utafanyika
-Kijiji kina
leseni 8 za uchimbaji wa madini
-Gharama za
ujenzi zitakuwa kubwa kutokana na jiografia ya mahali kijiji kilipo.
SIFA YA KIJIJI CHA KAMIKUSU
-Kijiji hiki
kipo km 20 kutoka barabara ya Mpanda-Uvinza
-Ni eneo ambalo
kipindio cha masika huwa tepetepe ambapo hakuna majengo makubwa yanayowezekana
kujengwa.
-Kipo katikati
ya mito miwili ambapo vyanzo hivyo vya maji vitaharibika.
-Kuna wakazi
wachache ambao watahitaji kulipwa fidia ya shilingi milioni 500 ili kupisha
ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri.
SIFA YA KIJIJI CHA MAJALILA
-Kuna eneo la
Heka 50 ambazo zimetolewa na wananchi bila fidia
-Eneo hilo
linafikika kwa urahisi kutokana na kuwa kandokando ya barabara kuu kutoka
Mpanda Kigoma.
-Kuna miradi wa
maji wa matenki mawili ambao umezinduliwa na mwenge wa uhuru.
-Wapo wananchi
zaidi ya 3000 watakaonufaika na mradi wa maji
-Kijiji cha
Majalila ni eneo ambalo lipo katika Mpango wa kunufaika na umeme wa REA(Wakala
wa umeme vijijini)
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo Mashama
Endelea kuhabarika na ‘’P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM’’
Comments