MGOGORO WA ARDHI KIJIJI CHA TUMAINI WILAYANI MPANDA WATOKOTA
Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
Serikali ya kijiji cha Tumaini
Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Wilayani Mpanda mkoani Katavi,imewalalamikia
watu wanaowatishia maisha kwa madai kuwa kijiji hicho kinataka kuwanyang’anya
ardhi yao.
Uongozi wa kijiji hicho umesema
kuwa,vitisho vya maisha wanavipata kutoka kwa baadhi ya viongozi waliokuwepo
madarakani katika kipindi cha uongozi uliopita ambapo takribani watu 10 wakiwemo
viongozi hao ndio wanadaiwa kuhodhi heka 2850 bila kufuata utaratibu wa sheria
za kijiji.
Kwa mjibu wa taarifa ya Muhtasari wa
kikao cha Halmsahuri ya Kijiji cha Tumaini kilichofanyika Aprili 16 mwaka huu,inaonesha
kuiwa miongoni mwa wanaotuhumiwa kuhodhi ardhi kwa kukiuka kifungu cha 8 cha sheria
ya ardhi ya kijiji namba ‘5’ ya mwaka 1999 ni Bw.Willium Midende mwenyekiti wa
zamani wa kijiji cha Tumaini anayedaiwa kuhodhi eneo la Heka 1500,Mwenyekiti wa
zamani wa Huduma za Jamii Bw.Kadumi Shija aliyehodhi eneo la heka 200 huku
Bw.Mashaka John Malale aliyekuwa katibu wa huduma za jamii kipindi cha uongozi
uliopita yeye kwa upande wake akituhumiwa kukimbia na nyaraka za serikali ya
kijiji na kuendelea kugawa ardhi kwa kutumia nyaraka hizo.
Hata hivyo watuhumiwa hao walikana
tuhuma dhidi yao ikiwemo kuwatishia maisha viongozi wa kijiji cha tumaini
ambapo mwenyekiti mstaafu Bw. Willium Midende amsema kuwa eneo analomiliki ni
ni kati ya heka 30-35 alizogawiwa na kijiji kihalali huku Bw.Kadumi shija yeye
akisema kuwa anamiliki Heka kati ya 25-35 alizopewa na kijjiji ambapo hata
hivyo kwa upande wake Bw.Mashaka John Malale aliyekuwa katibu wa huduma za
jamii akikanusha kukimbia na nyaraka za serikali na kuzitumia kugawa mashamba
ambapo alisema kuwa alizonazo ni taarifa zilizokataliwa katia mkutano wa kijiji
pekee.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata
ya Itenka Bw.Omary Hussein ambaye ametajwa kutopeleka muhtasari katika ngazi ya
Halmashauri ya wilaya kwa utatuzi wa migogoro amesema hajakataa kupeleka bali
anasubiri muhtasari wa kikao cha Halmshauri ya kijiji cha Tumaini.
Aidha Afisa Mtendaji wa Kata ya
Itenka Bw.Omary Hussein amesema,leo amepokea majina manne ya watu wanaodaiwa
kuwatishia maisha viongozi wa kijiji cha Tumaini na kuahidi kulishughulikia kwa
mjibu wa sheria.
Hata hivyo mwenyekiti wa Halmshauri
ya Wilaya ya Nsimbo Mh.Raphael Kalinga amesema yeye kama mwenyekiti wa halmshauri
ya Wilaya hajapokea taarifa ya mgogoro huo na ametoa wito kwa viongozi wa
kijiji cha Tumaini kupeleka taarifa za mgogoro huo ikiwa kuna tatizo ili
lishughulikiwe haraka.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo Mashama
Endelea kuhabarika na ‘’P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM’’
Comments