Posts

Showing posts from December 15, 2017

IGP SIRO AKIWA MKOANI KATAVI AMESISITIZA KUCHUKUA HATUA KALI ZA KISHERIA KWA WAHARIFU NCHINI

Image
Na.Issack Gerald Mkuu wa Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa ziarani Mkoani Katavi,amesema Jeshi la polisi litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu wote wanaojihusisha na uharifu mbalimbali ikiwemo Mauaji ya watu kwa imani za kishirikina. IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupokea ripoti ya mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kuhusu hali ya ulinzi,amani na usalama mkoani Katavi. Aidha Siro amesema uharifu Mkoani Katavi umepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na uharifu uliokuwepo katika miaka michache iliyopita. Wakati huo huo Kamanda Sirro ambaye aliwasili jana Mkoani Katavi kwa zaiara ya kikazi ya siku mbili,ameweka jiwe la msingi ujenzi wa zahanati ya jeshi la polisi Mjini Mpanda. Katika hatua nyingine IGP akiwa ameambatana na maafisa wa polisi kutoka makao makuu ya polisi nchini pamoja na waliopo Mkoani Katavi,amekagua na kuangalia maonesho mbalimbali ya namna jeshi la Polisi Mkoani...

SERIKALI IMEAGIZA KUSITISHA UVUVI ZIWA RUKWA

Image
Na.Issack Gerald SERIKALI mkoani  Rukwa imeagiza kulifunga ziwa Rukwa kwa muda usiojulikana kutokana na shughuli za uvuvi kuchangia kasi ya ugonjwa wa kipindupindu katika ziwa hilo. Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alitoa agizo hilo wakati akizingumza na wavuvi kwa lengo la kuwaeleza sababu za kulifunga ziwa hilo na kuzuia kabisa uvuvi kutoendelea. Alisema baada ya kukaa na wataalamu wa afya wamekubaliana kusitisha shughuli za uvuvi kwani zimekuwa chanzo kikubwa cha kuenea ugonjwa huo.  Alisema athari inayopatikana katika kambi hizo za uvuvi zitawaathiri walaji wa samaki wanaotokana ziwa hilo hasa waliopo Sumbawanga mjini kwani wanategemea samaki hapo Kama kutoweo na kuwataka walio waliopiga kambi katika ziwa hilo kwa ajili ya uvuvi waondoke mara moja kwani hawataruhusiwa kuingia ziwani kuendelea kuvua samaki.  Wakati huo huo aliagiza kufunguliwa maeneo maalumu kwa ajili ya kuwatibia wagonjwa  watakaopatikana kwani wasipofanya hivyo mlipuko wa ugonjwa huo...

UTAPELI NJE YA IKULU NDOGO MKOANI KATAVI

Image
Na.Issack Gerald Taasisi ya  kupambana na kuzuia  rushwa TAKUKURU  Mkoani  Katavi  imewakamata watu wawili ambao walijifanya kuwa ni maafisa watasisi hiyo na kwenda kupokea rushwa ya shilingi 400,000 karibu na majengo ya ikilu ndogo.  Watuhimiwa hao waliofahamika kwa Majina ya Nicodemo  Peter  pamoja na  Peter   Mwaninsawa  wakazi wa  Mtaa wa  Nsemlwa katika  Manispaa ya  Mpanda walijifanya maafisa wa takukuru na kutapeli fedha hizo. Tukio hilo lilitokea  jana   majira ya saa 4 asubuhi nje ya Ikulu  ndogo ya  Mkoa wa  Katavi  iliyopo  jirani na   ofisi ya TAKUKURU. Mkuu wa  Takukuru mkoani Katavi  John   Minyenya  amewaambia  wandishi wa  habari kuwa watuhumiwa  hao walikamatwa  kufuatia...