SERIKALI IMEAGIZA KUSITISHA UVUVI ZIWA RUKWA
Na.Issack Gerald
SERIKALI mkoani Rukwa imeagiza kulifunga ziwa Rukwa kwa
muda usiojulikana kutokana na shughuli za uvuvi kuchangia kasi ya ugonjwa wa
kipindupindu katika ziwa hilo.
Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alitoa agizo hilo wakati
akizingumza na wavuvi kwa lengo la kuwaeleza sababu za kulifunga ziwa hilo na
kuzuia kabisa uvuvi kutoendelea.
Alisema baada ya kukaa na wataalamu wa afya wamekubaliana
kusitisha shughuli za uvuvi kwani zimekuwa chanzo kikubwa cha kuenea ugonjwa
huo.
Alisema athari inayopatikana katika kambi hizo za uvuvi
zitawaathiri walaji wa samaki wanaotokana ziwa hilo hasa waliopo Sumbawanga
mjini kwani wanategemea samaki hapo Kama kutoweo na kuwataka walio waliopiga
kambi katika ziwa hilo kwa ajili ya uvuvi waondoke mara moja kwani hawataruhusiwa
kuingia ziwani kuendelea kuvua samaki.
Wakati huo huo aliagiza kufunguliwa maeneo maalumu kwa ajili ya
kuwatibia wagonjwa watakaopatikana kwani wasipofanya hivyo mlipuko wa
ugonjwa huo utaendelea kuongezeka na watu wengi zaidi wataendelea kupoteza
maisha kwa ugonjwa huo.
Mkuu huyo wa mkoa alifanya ziara katika kambi ya
wavuvi ya mererani iliyopo katika kijiji cha Ilanga Kata ya Muze Wilayani Sumbawanga
katika bonde la Ziwa Rukwa ambapo mpaka sasa Jumla ya wagonjwa 9 waliripotiwa
kuugua kipindupindu.
Awali akitoa taarifa ya ugonjwa huo Afisa afya wa Halmashauri ya
Wilaya ya Sumbawanga Plasidus Malapwa alisema ugonjwa huo ulibainika tangu
novemba 23 kutokana na mgonjwa aliyetoka kambi ya Lichili Kijiji cha Lichili
wilayani Momba Mkoani Songwe na kufia katika kambi ya kamchanga Kata ya Muze wilayani
Sumbawanga na kuanzia hapo wagonjwa walianza kuongezeka hali iliyosababisha
kuanzishwa kwa kambi nne kuzunguka ziwa Rukwa.
Naye Mganga mfawidhi wa Zahanati ya Muze Dkt Aron Mtolo alisema hatua
mbalimbali zimechukuliwa ili kudhibiti ugonjwa huo ikiwamo kufunga migahawa
michafu 8 kuvifungia vilabu vya kuuzia pombe ambapo pia mapipa manne na
debe tatu ya pombe ilimwagwa na wanywaji pombe 14 walilipishwa faini ya
shilingi 20,000 kila mmoja.
Chanzo:Gurian wa Rukwa Kwanza Blog
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments