RAIS MAGUFULI ATAKA VIONGOZI WA DINI KUJIEPUSHA NA MIGOGORO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa dini mbalimbali nchini kuhakikisha wanajiepusha na migogoro mbalimbali ambayo imekuwa ikiharibu sifa na heshima ya taasisi hizo za dini. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati alipohudhuria hafla ya kumweka wakfu na kumsimika Mchungaji Jackson Sosthenes Jackson kuwa Askofu wa tano wa Kanisa la Anglikana Dayosis ya Dar es Salaam. Kwa upande mwingine,Dkt.Magufuli amedai endapo mahali kwenye uponyaji wa mwili ukisikia kumeanza matatizo basi unapaswa kutazama jinsi taifa unaloliongoza roho zake zitakavyopotea. Misa ya kumsimika Askofu mteule Sosthenes imefanyika leo ikiongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Jacob Chimeledya. Mbali na Rais Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi wengine waliohudhuria ni mke wa Rais Maguli mama Janeth Mafuli,Rais mstaafu Benjamin Mkapa. Wengine ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Venance Mabeyo,Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba,Waziri wa ...