MAGUFULI AWATUNUKU MAOFISA 197 WA JWTZ
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maofisa wanafunzi 197 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Sherehe hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam ambapo maofisa hao wapya ni wa Tanzania na kutoka nchi marafiki waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha. Katia tukio hilo ambalo limepambwa na magwaride kutoka kwa Wanajeshi hao,limehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Kitaifa ambapo miongoni mwa waliotunukiwa kamisheni hizo wanawake ni 28 na waliobaki wakiwa ni wanaume. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED