BARAZA LA MADIWANI HALMSHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUFANYA KIKAO CHAKE KESHO,SHILINGI MIL.120 ZILIZOTUMIKA KINYUME NA MALENGO,BARAZA LA MADIWANI KUTOA TAMKO
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi BARAZA la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,kesho linatarajia kufanya kikao chake cha robo ya mwaka kwa mwaka 2016 ambapo masuala mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo kutoa tamko la kubadilishwa matumizi ya Shilingi milioni 120 zilizokuwa zitumike kununulia gari la Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri hiyo ambapo zilitumika kwa ajili ya Masuala ya mitihani. Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Hassan Mapengo(PICHA NA.Issack Gerald)