SHIRIKA LA UNHCR KESHO KUKABIDHI GARI KWA JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI KUSAIDIA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA
Na.Issack Gerald
Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
SHIRIKA la wakimbizi duniani UHNCR Mkoani
Katavi,kesho linatarajia kukabidhi gari kwa jeshi la Polisi Mkoani Katavi ili
kurahisisha shughuli za ulinzi na usalama za jeshi hilo.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya
habari,Afisa habari wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi Bw.Danny Kimario amesema
kuwa makabidhiano hayo yanatarajiwa kufanyika katika makazi mapya ya Mishamo
yaliyopo katika kata na Tarafa ya Mishamo Wilayani Tanganyika ambapo katika
eneo hilo pia zipo Ofisi za UNHCR.
Mwaka uliopita,jeshi la polisi mkoani
Katavi lilieleza kuwa na upungufu wa magari hali inayopelekea baadhi ya shughuli
za jeshi hilo kukwama.
Shirika la wakimbizi duniani UNHCR mbali
na tukio hilo linalotarajiwa kufanyika kesho,UNHCR pia limekuwa likisaidia vitendea kazi katika sekta
mbalimbali zikiwemo elimu,afya na sheria
ambapo katika sekta ya afya, hivi karibuni walikabidhi gari la kuhudumia
wagonjwa lenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 78 katika kituo cha afya Mishamo.
Endelea kuwa name kufahamu kitakachojili kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments