MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTELEKEZWA NA MUMEWE,WANAWAKE WALAANI
Wanawake wa Mtaa wa Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wamelaani vikali kitendo cha Abdalla Ibrahim Mkazi wa mtaa huo kumtelekeza mkewe Rosemary Robert Ismail mpaka kusababisha kifo chake kwa kutompatia huduma baada ya kuugua kwa muad mrefu. Wanawake hao wamesema kitendo ambacho amekifanya Bw.Ibrahimu ambaye ni mlinzi wa kampuni moja mjini Mpanda ni ukatiri wa hali ya juu.