Posts

Showing posts from December 13, 2017

RAIS MAGUFULI ATOA AHGIZO LA KIUCHUMI KWA BOT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka Benki Kuu ya Tanzania ( BOT ) kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni katika biashara na huduma hapa nchini ili kulinda nguvu ya fedha ya Tanzania na kukabiliana na uhalifu wa kifedha. Mhe.Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati akifungua tawi la benki ya CRDB-LAPF Dodoma na kubainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kuimarisha uchumi wa nchi. Aidha,Mhe.Rais Magufuli ameitaka BOT kuongeza usimamizi wa benki zinazoendesha shughuli zake hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha zinajiunga na mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki na kufuatilia kwa ukaribu utendaji wake wa kila siku ili ziwe na manufaa kwa nchi. Wakati huo huo Mhe.Rais Magufuli ameipongeza benki ya CRDB kwa kuendeshwa kwa ufanisi tangu ilipobinafsishwa kutoka Serikalini ambapo katika kipindi cha miaka 10 imelipa kodi serikalini kiasi cha Shilingi Bilioni 800,imetoa ajira kwa Watanzania 3,200,imetoa gawio Serikalini la Shilingi Bilio...

UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA MKOANI KATAVI,ZAIDI YA WANAFUNZI 9000 WAMEKOSA NAFASI YA KUIJUNGA KIDATO CHA KWANZA MAWAK 2018

Image
Na.Issack Gerald Zaidi ya wanafunzi 9000 waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mkoani Katavi wamekosa nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.  Akitangaza matokeo ya mtihani huo katika kikao maalumu cha uchaguzi wa wanafunzi Afisa Elimu mkoa wa Katavi Ernest Hinju amesema jumla watahiniwa 7,190 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kutwa. Aidha watahiniwa 162 hawakuweza kufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali hali iliyopelekea wadau wa elimu kujadili changamoto za kushuka kwa elimu, kwani kulinganisha na mwaka uliopita mkoa wa Katavi umeshika nafasi ya 9 kitaifa kutoka nafasi ya 2 mwaka uliopita  Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Katavi Bw. Gideon Marandu amezitaka halmashauri zote kuhakikisha wanafunzi waliokosa nafasi wanapata nafasi ifikapo Februari mwaka 2018. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WANAWAKE WAJAWAZITO WILAYANI MPANDA WANALAZIMIKA KUBEBA MAJI KUTOKA NYUMBANI MPAKA ZAHANATI KWA AJILI YA USAFI WAKATI WA KUJIFUNGUA

Na.Issack Gerald Wanawake wote wajawazito katika kijiji cha Mtambo kata ya Katumba Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi, wanalazimika kubeba maji kutoka nyumbani na kuyapeleka katika zahanati ya Mtambo iliyopo kijijini hapo ili yatumike wakati wakijifungua. Mganga mfawidhi wa zahanti hiyo Dkt.Daud Mashama amesema wanawake wajawazito wasi pokuja na maji hulazimika kufuata maji mto Kalutonya uliopo umbali wa kilomita 8 kutoka zahanati ya Mtambo. Kaimu afisa Mtendaji wa kata ya Katumba Bi.Lucy Kagine amekiri kuwepo kwa tatizo la maji katika kijiji cha Mtambo huku akisema mara kwa mara kila wanapochimba visima upatikanaji wa maji umekuwa mgumu. Kwa upande wake Katibu wa kijiji cha Mtambo Bw.Fenias Fulujensi pamoja na mambo mengine amesema wanasubiri uwekaji wa mitambo katika kisima kilichochimbwa ili kusukuma maji. Kwa mjibu wa wakazi wa kijiji cha Mtambo,zahanati ya Mtambo ilijengwa miaka ya 1992 ambapo hata hivyo Juhudi za kutafuta uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya...