SERIKALI YA WILAYA YA MLELE KWENDA KWA WAZIRI KUPATA UHAKIKA LINI HOSPITALI ITAJENGWA
Na.Issack Gerald-MLELE SERIKALI ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, imesema inatarajia kwenda kumuona Waziri wa Afya ili kupata uhakika lini wananchi waliotoa ardhi yao kujengwa hospitali ya wilaya hiyo watalipwa fidia zao.