Posts

Showing posts from March 30, 2018

MKUU WA WILAYA AIBULIWA NA SHULE KUITA WAGANGA KUTOKA KONGO

Image
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mohamed Mtanda ametolea ufafanuzi suala la shule ya Msingi Kabwe kuita waganga wa kienyeji kutoka Kongo ili kutatua tatizo la kishirikina linaloikabili shule hiyo.` Mtanda amesema ni kweli alipokea simu kutoka kwa Mkuu wa shule hiyo kumuelezea matatizo yao hapo shuleni na lengo walilofikia serikali ya kijiji ili kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara. Licha ya hayo,mkuu wa wilaya hiyo amesema yeye kama kiongozi wa serikali ni kulichukua tatizo hilo kitaalam kwa kupeleka madaktari ambao watatafuta njia sahihi ya kutibu wanafunzi hao na sio kuruhusu mambo ya kishirikina ingawa hawezi kuwakataza wazee wa kijiji hicho kwani anaheshimu mila zao. Wanafunzi wa kike wa shule ya msingi Kabwe iliyopo Wilayani Nkasi mkoani Rukwa wanakabiliwa na tatizo la kiafya la kuanguka,kuzimia na kupiga kelele jambo ambalo wakazi wa eneo hilo wanahisi linatokana na ushirikina na kuamua kutafuta waganga wa kienyeji ili kutafuta ufumbuzi. Chanzo:ea...

ASKOFU NYAISONGA ATAKA WAKRISTO WATENDE MEMA

Image
Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga Katika maadhimisho ya siku ya Ijumaa kuu kwa wakristo,Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda Mkoani Katavi   Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga amewataka waumini wa kikristo kuendelea kutenda kutenda mema kama walivyofanya katika kipindi cha mfungu wa Kwaresma. Askofu Nyaisonga ametoa wito huo leo katika adhimisho misa takatifu ya Ijumaa kuu katika ibada ambayo imefanyika katika Kanisa kuu la Bikira Maria Emakulata Jimbo la Mpanda. Kwa upande wao waumini wa kanisa hilo wamesema kipindi cha Kwaresma ni kipindi cha kutafakari wema ambao mungu ameuonesha kwao na hivyo kutakiwa kutenda hivyo hivyo kwa wenye uhitaji. Ijumaa Kuu ni siku maalumu ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa ambapo inatanguliwa na Alhamisi Kuu. Sikukuu ya pasaka kwa mwaka 2018 inatarajiwa kuadhimishwa Aprili mosi mwaka huu. Ijumaa kuu kitaifa imeadhimish...

IJUMAA KUU

Image
Ijumaa Kuu  ni  siku  maalumu ya  mwaka  ambayo  wafuasi  wengi wa  Yesu Kristo  wanaadhimisha  kifo  chake  msalabani  ambacho kilitokea nje ya kuta za  mji  wa  Yerusalemu  siku ya  Ijumaa . Kadiri ya  Injili  ya  Mtume Yohane ,kesho yake ilikuwa  Sabato  na pia  Pasaka ,jambo lisilotokea kwa kawaida. Kwa sababu hiyo  wataalamu  mbalimbali wanakadiria ilikuwa tarehe  7 Aprili   30 . Ijumaa kuu ni sehemu ya  Juma Kuu  linaloanza kwa adhimisho la  Yesu  kuingia mji huo akishangiliwa kama  mfalme wa Wayahudi  (yaani  Masiya  au  Kristo ).Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa  wiki , yaani  Jumapili ya matawi . Ijumaa kuu ni pia sehemu ya  siku tatu kuu za Pasaka  zinazoadhimisha mateso na  kifo chake  ( Ijumaa ), kulala  kaburini  ( Jumamosi ), na hatim...