MKUU WA WILAYA AIBULIWA NA SHULE KUITA WAGANGA KUTOKA KONGO
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mohamed
Mtanda ametolea ufafanuzi suala la shule ya Msingi Kabwe kuita waganga wa
kienyeji kutoka Kongo ili kutatua tatizo la kishirikina linaloikabili shule
hiyo.`
Mtanda amesema ni kweli alipokea simu
kutoka kwa Mkuu wa shule hiyo kumuelezea matatizo yao hapo shuleni na lengo
walilofikia serikali ya kijiji ili kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa
likijitokeza mara kwa mara.
Licha ya hayo,mkuu wa wilaya hiyo
amesema yeye kama kiongozi wa serikali ni kulichukua tatizo hilo kitaalam kwa
kupeleka madaktari ambao watatafuta njia sahihi ya kutibu wanafunzi hao na sio
kuruhusu mambo ya kishirikina ingawa hawezi kuwakataza wazee wa kijiji hicho
kwani anaheshimu mila zao.
Wanafunzi wa kike wa shule ya msingi
Kabwe iliyopo Wilayani Nkasi mkoani Rukwa wanakabiliwa na tatizo la kiafya la
kuanguka,kuzimia na kupiga kelele jambo ambalo wakazi wa eneo hilo wanahisi
linatokana na ushirikina na kuamua kutafuta waganga wa kienyeji ili kutafuta
ufumbuzi.
Chanzo:eatv
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments