IJUMAA KUU
Ijumaa Kuu ni siku maalumu ya mwaka ambayo wafuasi wengi
wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho
kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu siku
ya Ijumaa.
Kadiri ya Injili ya Mtume Yohane,kesho
yake ilikuwa Sabato na
pia Pasaka,jambo
lisilotokea kwa kawaida. Kwa sababu hiyo wataalamu mbalimbali
wanakadiria ilikuwa tarehe 7 Aprili 30.
Ijumaa kuu ni
sehemu ya Juma Kuu linaloanza
kwa adhimisho la Yesu kuingia
mji huo akishangiliwa kama mfalme wa Wayahudi (yaani Masiya au Kristo).Adhimisho
hilo linafanyika mwanzoni mwa wiki, yaani Jumapili ya matawi.
Ijumaa kuu ni
pia sehemu ya siku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha
mateso na kifo chake (Ijumaa),
kulala kaburini (Jumamosi),
na hatimaye kufufuka kwa utukufu (Jumapili),
kwa ufupi: Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka.
Jana ilikuwa Alhamisi KUU
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments