RAIS AWAPANDISHA VYEO MAAFISA WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo Aprili 12,2018 amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) katika vyeo mbalimbali. Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo,Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Paul Massao kuwa Luteni Jenerali.