LEO NI KUMBUKUMBU YA MIAKA 34 YA KIFO EDWARD SOKOINE HISTORIA YAKE IKO HAPA
Edward
Moringe Sokoine (1938 - 12 Aprili 1984) alikuwa mwanasiasa kutoka
nchi ya Tanzania.
Aliwahi
kuwa Waziri Mkuu mara mbili,tangu tarehe 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980,tena tangu
tarehe 24 Februari 1983 hadi kifo chake,alipofariki
kufuatana na ajali ya
gari.
Uongozi
wake ulionekana kuwa wa mfano kwa jinsi alivyokuwa na uadilifu na kufuatilia utendaji kazi
huku akikemea ulaji rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.
Upande
wa dini,alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki,tena
mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.
Sokoine
alifariki kwa ajali ya gari wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam.
Wengi wanashuku ajali hiyo kuwa ilipangwa.
Kifo
chake kilileta majonzi makubwa kwa Watanzania wa kawaida ambao walikuwa
wanamtarajia kuwatetea wanyonge na kuinua hali ya maisha yao.
Chuo cha Kilimo
na Mifugo Morogoro kilipewa jina la "Chuo cha Kilimo cha
Sokoine"ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Sokoine.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments