Posts

Showing posts from December 2, 2017

MBUNGE NASSARI:NIMENUSURIKA KUUWAWA KWA RISASI USIKU

Image
Mbunge wa Jimbo la arumeru Mashariki Joshua Nassari, amevamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha na kunusurika kupigwa na risasi ambazo zimeua mbwa wake. Mh.Joshua Nassari Katika ukurasa wake wa twitter,Nassari ameandika ujumbe akitoa taarifa kuwa watu hao wamevamia nyumbani kwake usiku wakiwa na silaha za moto ambazo wamewafyatulia mbwa wake. Mbunge huyo mara kadhaa amekuwa akiripoti katika mitandao ya kijamii kuwa amekuwa atishiwa kuuawa mara kwa mara. Hakuna kauli ya jeshi la polisi ambayo imetolewa kuzungumzia tukio hilo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA IMEKANUSHA UWEPO WA PEMBEJEO FEKI

Image
Na.Issack Gerald Halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imekanusha kuhusu uwepo wa pembejeo feki zinazosambazwa na kutumika katika msimu huu wa kilimo. Hayo yamesemwa na afisa kilimo wa halimashauri hiyo Bw. Fabian Kashindye ambapo ameeleza kuwa kitisho hicho ni sawa na propaganda. Zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa Tanzania hutegemea kilimo katika kuendesha maisha na kipato cha kaya,wengi wao ni kutoka vijijini ambao hukabiliwa na elimu duni kuhusu kilimo bora. Hivi karibuni Waziri wa Kilimo,Dk Charles Tizeba ameitaja mikoa ya Rukwa,Njombe,Iringa,Songwe na Mbeya kuongoza kwa kuuza mbegu feki za mahindi na kusababisha madhara makubwa kwa wakulima, ikiwemo uzalishaji mdogo wa zao hilo Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAKAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO WAMELALAMIKA KUNYANG’ANYWA GARI LA WAGONJWA,HALMASHAURI YATOA UFAFANUZI

Image
Na.Issack Gerald Wakazi wa kata ya Katumba Halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wameilalamikia Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa madai kuwa halmashauri hiyo imewanyanga’anya gari la wagonjwa ambalo limekuwa likitoa huduma kwa wagonjwa katika kata hiyo. Wamesema kuwa wamenyang’anywa gari kwa madai kuwa wakazi wa Katumba hawana dereva wa kuendesha gari hilo. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Mh.Raphael Kalinga amekanusaha kuwanyang’anya gari la wagonjwa wakazi wa Kata ya Katumba ambapo amesema lipo kwenye matengenezo baada ya kuharibika. Aidha Kalinga amesema suala la kuharibika kwa gari hilo limekwishatolewa ufafanuzi kuanzia kwa viongozi wa Halmashauri,Mkoa hadi ngazi ya wizara. Kata ya Katumba ina vijiji 16 na zaidi ya wakazi elfu hamsini wanaotegemea huduma ya gari hilo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED