HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA IMEKANUSHA UWEPO WA PEMBEJEO FEKI

Na.Issack Gerald
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imekanusha kuhusu uwepo wa pembejeo feki zinazosambazwa na kutumika katika msimu huu wa kilimo.
Hayo yamesemwa na afisa kilimo wa halimashauri hiyo Bw. Fabian Kashindye ambapo ameeleza kuwa kitisho hicho ni sawa na propaganda.
Zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa Tanzania hutegemea kilimo katika kuendesha maisha na kipato cha kaya,wengi wao ni kutoka vijijini ambao hukabiliwa na elimu duni kuhusu kilimo bora.
Hivi karibuni Waziri wa Kilimo,Dk Charles Tizeba ameitaja mikoa ya Rukwa,Njombe,Iringa,Songwe na Mbeya kuongoza kwa kuuza mbegu feki za mahindi na kusababisha madhara makubwa kwa wakulima, ikiwemo uzalishaji mdogo wa zao hilo

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA