WANNE MBARONI KATAVI AKIWEMO MWENYE NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.60
Na.Issack Gerald-MLELE Jeshi la Polisi Wilayani Mlele Mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya wanyama Pori (TANAPA) ,linawashikilia watu wanne akiwemo mmoja ambaye amekamatwa na jino moja na mikia miwili ya Tembo vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 60.