WANNE MBARONI KATAVI AKIWEMO MWENYE NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.60
Na.Issack Gerald-MLELE
Jeshi
la Polisi Wilayani Mlele Mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa
Hifadhi ya Taifa ya wanyama Pori (TANAPA) ,linawashikilia watu wanne akiwemo mmoja ambaye amekamatwa na
jino
moja na mikia miwili ya Tembo vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 60.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri
Kidavashari amemtaja ambaye amekamatwa na nyara hizo za serikali kuwa ni Haruna
Exavery (20) mkazi wa kata ya Sitalike.
Aidha Kidavashari amesema,wamewakamata Juma
Kapongo (55),Amos Gerald Kapongo (20) na Haruna Exavery Sikazwe(20), wote
wakazi wa Kata ya Sitalike wakiwa na silaha moja aina ya gobore yenye risasi
moja kinyume na sheria.
Mbali na watuhumiwa hao kufikishwa
mahakamani upelelezi utakapokamilika,Kamanda Kidavashari amewataka wanakatavi kufanya
shughuli halali za kujipatia kipato na kutoendelea na vitendo vilivyo kinyume
na sheria.
Comments