Rangi ya kijivu ndipo Wilaya ya Kasulu inapopatikana Mkoani Kigoma MTOTO anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya wiki tatu na Mwezi mmoja wilayani Kasulu mkoani Kigoma ameokotwa katika migomba alipotelekezwa na mwanamke asiyejulikana na kutokomea kusiko julikana. Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nyakitonto wilayani humo Bw Julius Baligela amesema mtoto huyo wa njisi ya kike ameokotwa kwenye migomba jirani na mahame ya mtu mmoja akiwa amefungwa kanga. Bw Baligela ameeleza kuwa majira ya saa kumi na mbili asubuhi wasamalia wema walitoa taarifa wa uongozi na kisha kumpeleka hospitali kwa matibabu baada ya taratibu za kipolisi kukamilika na halamshauri imetoa gari kusafirisha mtoto kuyo kituo cha kulelea watoto Matyazo Kigoma. Aidha Kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji cha Nyakitonto kwa kushirikiana na wananchi inaendelea kufanya uchunguzi kumbaini mwanamke aliyehusika na kitendo hicho. Habarika zaid...