MTOTO MCHANGA AOKOTWA SHAMBA LA MIGOMBA BAADA YA KUTELEKEZWA NA MWANAMKE ASIYEJULIKANA- Julai 11-2017.
Rangi ya kijivu ndipo Wilaya ya Kasulu inapopatikana Mkoani Kigoma |
MTOTO anayekadiriwa
kuwa na umri wa kati ya wiki tatu na Mwezi mmoja wilayani Kasulu mkoani Kigoma
ameokotwa katika migomba alipotelekezwa na mwanamke
asiyejulikana na kutokomea kusiko julikana.
Mwenyekiti wa
serikali ya kijiji cha Nyakitonto wilayani humo Bw Julius Baligela amesema mtoto huyo
wa njisi ya kike ameokotwa kwenye migomba jirani na mahame ya mtu mmoja akiwa
amefungwa kanga.
Bw Baligela
ameeleza kuwa majira ya saa kumi na mbili asubuhi wasamalia wema walitoa
taarifa wa uongozi na kisha kumpeleka hospitali kwa matibabu baada ya taratibu
za kipolisi kukamilika na halamshauri imetoa gari kusafirisha mtoto kuyo kituo
cha kulelea watoto Matyazo Kigoma.
Aidha Kamati ya
ulinzi na usalama ya kijiji cha Nyakitonto kwa kushirikiana na
wananchi inaendelea kufanya uchunguzi kumbaini mwanamke aliyehusika
na kitendo hicho.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments