WAKAZI WILAYANI MLELE WATAKA MIFUGO IDHIBITIWE KULINDA MAZINGIRA-Julai 11,2017
WAKAZI wa mtaa wa Katandala kata ya Majimoto Mkoani Katavi,wameuomba uongozi kushughulikia uzururaji holela wa mifugo.
Wakizungumza na Mpanda Radio Fm,wakazi hao wamesema
kuwa,wanyama wakiwemo nguruwe na mbuzi huzurura ovyo katika makazi ya watu na
hivyo kupelekea uharibifu wa mazingira.
Aidha wameuomba uongozi kuhakikisha wanawapa zaidi
elimu wananchi ili kuhakikisha wanajenga mazizi ya mifugo kuepuka migogoro isiyo
ya lazima.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Katandala
Bw.Isaya Pausanda,amekili kuwepo kwa adha hiyo na amewataka wafugaji wote
kuhakikisha wanafungia mifugo yao katika Mazizi.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments