KUHUSU MADARASA YA WANAFUNZI WENYE WALEMAVU SHULE YA ,MSNGI AZIMIO,SASA SARAKASI TUPU KATI YA MANISPAA YA MPANDA NA MKANDARASI
Na.Issack Gerald-Mpanda Kamati ya shule ya msingi Azimio katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imezuia malipo ya shilingi Milioni tano (5,000,000) kwa mkandarasi anayefahamika kwa jina la Paul Luguyashi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwandoya Investment aliyejenga madarasa mawili ya watoto wenye ulemavu katika shule hiyo kwa madai kuwa sehemu ya majengo hao aliyoambiwa kufanya marekebisho ya majengo hayo hakutekeleza.