KUHUSU MADARASA YA WANAFUNZI WENYE WALEMAVU SHULE YA ,MSNGI AZIMIO,SASA SARAKASI TUPU KATI YA MANISPAA YA MPANDA NA MKANDARASI
Na.Issack Gerald-Mpanda
Kamati ya shule ya msingi Azimio katika
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imezuia malipo ya shilingi Milioni tano (5,000,000)
kwa mkandarasi anayefahamika kwa jina la Paul Luguyashi ambaye ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Mwandoya Investment aliyejenga madarasa mawili ya watoto wenye
ulemavu katika shule hiyo kwa madai kuwa sehemu ya majengo hao aliyoambiwa kufanya
marekebisho ya majengo hayo hakutekeleza.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio Fm,Makamu mwenyekiti wa
kamati hiyo Bw.Patrick Julius Mbasha amesema,licha ya Mhandisi wa Manispaa ya Mpanda kuidhinisha malipo kufanyika
na pesa hiyo kuingizwa katika akaunti benki shule ya msingi Azimio,kamati haitaidhinisha
pesa hiyo kukabidhiwa kwa mkandarasi huyo hadi hapo atakapofanya marekebisho.
Bw.Mbasha amesema,kucheleweshwa kwa
malipo ya fedha hiyo kumetokana na mkandarasi kutofanya marekebisho kama
alivyoelekezwa na watalaamu wa ujenzi kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi huyo wa Kampuni
ya Mwandoya Investment amesema,marekebisho aliyotakiwa kuyafanya
alikwishamaliza na kilichokuwa kimesalia ni malipo pekee na ndiyo maana alipewa
nakala ya barua ya Februari 8 mwaka huu na kamati kuagizwa kumlipa shilingingi
milioni Tano iliyoingizwa katika akaunti benki ya shule.
Hata hivyo kutokana na hali
hiyo,mkandarasi hiyo amesema, kutokana na ucheleweshaji wa kumlipa psea yake mpaka
sasa pamoja na riba ya malimbikizo ya pesa yote imefikia karibu milioni 33
suala ambalo kamati ya shule imesema haitambui kiasi hicho cha fedha.
Aidha Mkandarasi huyo ameenedelea
kusisitiza kufunga madarasa hayo mpaka atakapoliwa pesa yake na akafafanunua
kuwa ikiwa suala hili halitakwisha,atalipeleka Wizara ya Tawala za mikoa na
serikali za mitaa TAMISEMI kwa hatua
zaidi.
Naye Kaimu mkurugenzi Manispaa ya
Mpanda Bw.Hamisi Mkele,amesema suala hilo limebaki mikononi mwa kamati ya shule
kulipwa pesa iliyoidhinishwa na Manispaa na akaongeza kuwa ikiwa mkandarasi
anadai milioni 33 ikiujumuisha pamoja na riba basi afike Ofisini ambapo kwa
mjibu wa maelezo ya mkandarasi,siyo mara ya kwanza kuzungumza nao suala la
nyongeza ya riba.
Madarasa hayo mawili ya watoto wenye
ulemavu wengi wao wakiwa wa kutosikia yalikamilika kujengwa mwaka 2014 huku
maelewano yakiwa ni Shilingi milioni 33 na awali zikawa zimelipwa milioni 26 na
kusalia milioni 7 hadi alipofunga madarsa hayo mwaka 2014 akishinikiza kulipwa
pesa anayodai.
Wanafunzi hao kuanzia darasa la kwanza
hadi la saba kwa miaka 7 tangu mwaka 2007,wanafundishiwa katika darasa
moja,ubao mmoja na wakati mwingine walimu zaidi ya watatu kufundisha kwa wakati mmoja.
Comments