KWA MWAKA 2017 WAPO WENGI WALIOTUMBULIWA NA RAIS MAGUFULI,HAWA NI BAADHI YA VIGOGO
Katika mwaka 2017, mambo mengi yametokea ambayo yametikisa nchi kuanzia kwenye nyanja ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na hata kiutamaduni. Imekuwepo mijadala mikubwa sana kuanzia kwenye ajali za barabarani, uchumi wa nchi, utawala, na mambo mengine yanayogusa maisha ya wananchi. Rais Dkt John Magufuli Wakati zikiwa zimesalia siku 6 mwaka 2017 kuisha, na mjadala sasa ukiwa ni sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya na suala la Wachagga kurudi makwao, tutakuwa hatujautendea haki kama, japo kwa ufupi hatutakumbushana masuala yaliyotokea kwenye siasa kwa mwaka huu. Mwaka huu, neno “Kutumbua” lilishika kasi sana. Hii ni kutokana na Rais Magufuli ambaye alisema amejipa kazi ya kutumbua majipu, kuwafuta kazi viongozi ambao kwake yeye aliona hawaendani na kasi yake au kutokana na sababu nyingine yoyote. Idadi ya waliotumbuliwa ni wengi, na katika mjadala wetu wa leo, tutaangazia vigogo 12 waliotumbuliwa tangu Januari 1, 2017. 1. Mhandisi Felchesmi Mramba. Januari Mosi 2017, R...