Posts

Showing posts from October 13, 2017

SHEIKH PONDA AJISALIMISHA CENTRAL POLISI

Image
Sheikh Issa Ponda Katibu mkuu wa baraza la mashirika ya kiislamu nchini Tanzania Sheikh Issa Ponda amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Central.

VITUO VYA AFYA MKOANI RUKWA VIMELAUMIWA KUTOKOPA FEDHA KUTOKA MFUKO WA BIMA YA TAIFA YA AFYA

VITUO vya afya vya serikali mkoani Rukwa vimelaumiwa kwa kushindwa  kutumia fursa ya kuomba mikopo katika mfuko wa bima ya afya ya Taifa kwa ajili ya kununua madawa,vitendanishi pamoja na ukarabati wa majengo badala yake vituo vya watu binafsi na madhehebu ya dini ndio wamekuwa wa kinufaika na fursa hiyo. 

WANANCHI MKOANI KATAVI WAASWA KUMUENZI NYERERE KWA KUDUMISHA AMANI

Image
Ikiwa kesho ni kilele cha mbio za mwenye wa uhuru na kumbukumbu ya kifo cha Hayati Julius Nyerere,wakazi Mkoani Katavi wamesema kumbukumbu ya miaka 18 tangu kifo cha hayati Baba wa Taifa  Mwl.Julius Kambarage Nyerere inafaa kutumika kuyaenzi kwa kudumisha amani na mshikamano .

KILELE WIKI YA VIJANA,VIJANA MKOANI KATAVI WASHAURIWA KUJIAJIRI

BAADHI ya vijana katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wamewashauri vijana wenzao kufanya kazi kwa bidii kama sehemu ya kuadhimisha wiki ya vijana hapa nchini.

RAIS MAGUFULI AWASILI ZANZIBAR KUJIANDAA KUZIMAMWENGE WA UHURU

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli,amewasili Zanzibar kwa ajili kuhitimisha kilele cha mbio za mwenge wa uhuru hapo kesho. Rais Dkt John Maguli akishuka katika uwanja wa ndege wa Amani Rais Magufuli mara baada ya kuwasili visiwani Zanzibar amepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.