Posts

Showing posts from April 7, 2018

AJALI YA BODABODA NA GARI KATAVI

Image
Dereva wa pikipiki maarufu kama Boda boda ambaye  jina lake halikufahamika Mara Moja Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,amejeruhiwa baada ya pikipiki yenye namba za usajil Mc 743 BQG aliyokuwa akiendesha kuligonga kwa Nyuma gari aina ya Raum eneo la Buzogwe njia mbili. Mashuhuda wa tukio hilo  ambalo limetokea leo wamesema,dereva huyo alikuwa akijaribu kuingia barabara kuu ya Buzogwe ndipo akawa amegongana na  Gari lenye namba za usajili T498 CFU.  Kwa mjibu wa mashuhuda hao,madereva wote wawili walikuwa na makosa baada ya wote kutozingatia sheria za usalama barabarani. Hata hivyo dereva wa gari hilo ambalo limegongana na pikpiki ametokomea kusikojulikana baada ya kutoonekana eneo la tukio baada ya Ajali hiyo kutokea. Hata hivyo askari polisi wa usalama barabarani ambao walifika eneo la tukio,wamekataa kuzungumzia tukio hilo wakidai wao siyo wasemaji. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com  

RAIS MAGUFULI ATOA SAA 24 KWA IGP AKIZINDUA NYUMBA 31 ZA POLISI

Image
Rais Dkt.John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Simon Sirro kuhakikisha inapofika kesho Aprili 8, 2018 awe ameshawaingiza askari Polisi walionguliwa nyumba zao hapo awali katika nyumba mpya ambazo zimezinduliwa hii leo. Dkt.Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati alipokuwa anazungumza muda mchache alipomaliza kuzindua nyumba za askari zilizojengwa mkoani Arusha. Amesema anawapa pole kwa majanga yaliyotokea ya kuunguliwa moto,huku akiwapongeza wadau mbalimbali waliojitolea kwa mioyo yao katika ujenzi wa nyumba hizo. Aidha amesema anataka wale wale walionguliwa ndio waingie humo katika nyumba hizo ambapo ameeleza kuwa nyumba kuugua imedhihirisha makazi ya nyumba za polisi yalivyokuwa mabovu. Jumla ya nyumba 31 za polisi   mjini Arusha zimezinduliwa tayari kwa ajili ya polisi. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com  

DC AAGIZA WALIOKAIDI KUFANYA USAFI WAKAMTWE

Image
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wafanyabiasha wa soko la Buzogwe katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda baada ya kukaidi agizo la kufanya usafi katika maeneo ya soko hilo. DC Lilian Matinga Picha na Issack Gerald Matinga ametoa agizo hilo leo wakati akishiriki zoezi la usafi katika soko la Buzogwe akiwa ameambatana na maafisa wa jeshi la polisi pamoja na watumishi wakiwemo watumishi wa umma. Amesema kuwa katika soko hilo hakuna aliyefanya usafi zadi ya mwenyekiti wa soko ambapo amesema watakaochukuliwa hatua watawajibishwa kwa kulipa faini ya shilingi 50,000 ikiwezekana hata kupelekwa mahabusu. Baadhi ya wananchi ambao wameshiriki zoezi la usafi wamesema kama serikali itaendelea kuhamasisha usafi mara kwa mara hakutakuwa na hofu ya magonjwa ya mlipuko. Jana mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga,aliagiza watumishi wa umma na wananchi kushiriki katika zoezi la usafi kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 46 ya k...

KATAVI WAFANYA USAFI WAADHIMISHA KIFO CHA KARUME

Image
Serikali ya Mkoa wa Katavi umefanya zoezi la usafi kama sehemu ya kuadhimisha miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar   Hayati Sheikh Abeid Amani Karume. Katika taarifa iliyokuwa imetolewa jana na Afisa Habari wa Manispaa ya Mpanda Pius Donald alikuwa amebainisha maeneo yanayofanyiwa usafi kuwa ni pamoja na maeneo ya hospitali,sokoni na stendi kuu. Serikali imekuwa ikiwataka watanzania kufanya usafi wa hali ya juu katika maeneo yao ili kuendelea kuwa salama ikiwemo kuepuka maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama kipindipindu ambapo imekuwa ikifikia hatua ya kuchukua hatua kali za kisheria wa watu wanaokaidi kufanya usafi katika maeneo yao. Hayati Sheikh Abeid Amani Karume alizaliwa mwaka 1905 na alifariki dunia tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi hadaharani wakati akicheza bao huko Zanzibar. Habari zaidio ni  www.p5tanzania.blogspot.com  

MBUNGE WA SUMBAWANGA ATISHIA KUZICHAPA KAVUKAVU BUNGENI

Image
Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aesh Hillary (CCM), ameeleza kushangazwa na kitendo cha Serikali kutenga Sh bilioni 15 kati ya Sh bilioni 80 zilizoombwa na Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) na kwamba iwapo serikali itafunga mipaka ya nchi ili chakula kisiuzwe nje, watashikana mashati bungeni. Akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma jana Ijumaa aprili 6, Aesh alisema fedha hizo zilizotengwa zinatosha kunua mahindi Wilaya ya Sumbawanga pekee. “Kama mkishindwa kununua haya mahindi msifunge mipaka, mwaka jana mmefunga mkaja kufungua wakati muda umekwenda na kuweka masharti magumu, nawaambia safari hii mkishindwa kununua mkafunga mipaka tutashikana mashati humu ndani. “Siyo kazi ya mkulima kuhakikisha nchi haina njaa ni kazi ya Serikali, nashangaa huku mnasema tu tumbaku na pamba, bila mahindi huyo mkulima hawezi kulima hayo mazao yake,” alisema Aesh. Aeshi pia amezungumzia watumishi wenye elimu ya darasa la saba kufukuzwa kazi akise...