RAIS MAGUFULI ATOA SAA 24 KWA IGP AKIZINDUA NYUMBA 31 ZA POLISI
Rais Dkt.John Magufuli amemuagiza
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Simon Sirro kuhakikisha inapofika kesho Aprili 8,
2018 awe ameshawaingiza askari Polisi walionguliwa nyumba zao hapo awali katika
nyumba mpya ambazo zimezinduliwa hii leo.
Dkt.Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati
alipokuwa anazungumza muda mchache alipomaliza kuzindua nyumba za askari
zilizojengwa mkoani Arusha.
Amesema anawapa pole kwa majanga yaliyotokea
ya kuunguliwa moto,huku akiwapongeza wadau mbalimbali waliojitolea kwa mioyo
yao katika ujenzi wa nyumba hizo.
Aidha amesema anataka wale wale
walionguliwa ndio waingie humo katika nyumba hizo ambapo ameeleza kuwa nyumba
kuugua imedhihirisha makazi ya nyumba za polisi yalivyokuwa mabovu.
Jumla ya nyumba 31 za polisi mjini Arusha zimezinduliwa tayari kwa ajili ya
polisi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments