MBUNGE WA SUMBAWANGA ATISHIA KUZICHAPA KAVUKAVU BUNGENI
Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aesh
Hillary (CCM), ameeleza kushangazwa na kitendo cha Serikali kutenga Sh bilioni
15 kati ya Sh bilioni 80 zilizoombwa na Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) na
kwamba iwapo serikali itafunga mipaka ya nchi ili chakula kisiuzwe nje, watashikana
mashati bungeni.
Akichangia hotuba ya Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma jana Ijumaa aprili 6,
Aesh alisema fedha hizo zilizotengwa zinatosha kunua mahindi Wilaya ya
Sumbawanga pekee.
“Kama mkishindwa kununua haya mahindi
msifunge mipaka, mwaka jana mmefunga mkaja kufungua wakati muda umekwenda na
kuweka masharti magumu, nawaambia safari hii mkishindwa kununua mkafunga mipaka
tutashikana mashati humu ndani.
“Siyo kazi ya mkulima kuhakikisha
nchi haina njaa ni kazi ya Serikali, nashangaa huku mnasema tu tumbaku na
pamba, bila mahindi huyo mkulima hawezi kulima hayo mazao yake,” alisema Aesh.
Aeshi pia amezungumzia watumishi
wenye elimu ya darasa la saba kufukuzwa kazi akisema mmoja wa
Madereva waliofukuzwa kazi
alimwendesha mpaka Waziri Mkuu Mstaafu (hakutaja jina la waziri huyo).
“Huyu dereva alikuwa amebakisha miaka
mitano tu astaafu, sasa hivi mmemfukuza kazi hana cha kufanya, suala hili
mliangalie upya,” alisema.
Habari zaidio ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments