AJALI YA BODABODA NA GARI KATAVI
Dereva wa pikipiki maarufu kama Boda
boda ambaye jina lake halikufahamika
Mara Moja Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,amejeruhiwa baada ya pikipiki yenye
namba za usajil Mc 743 BQG aliyokuwa akiendesha kuligonga kwa Nyuma gari aina
ya Raum eneo la Buzogwe njia mbili.
Mashuhuda wa tukio hilo ambalo limetokea leo wamesema,dereva huyo alikuwa akijaribu kuingia barabara kuu ya Buzogwe ndipo akawa amegongana na Gari lenye namba za usajili T498 CFU.
Kwa mjibu wa mashuhuda hao,madereva
wote wawili walikuwa na makosa baada ya wote kutozingatia sheria za usalama
barabarani.
Hata hivyo dereva wa gari hilo ambalo
limegongana na pikpiki ametokomea kusikojulikana baada ya kutoonekana eneo la
tukio baada ya Ajali hiyo kutokea.
Hata hivyo askari polisi wa usalama
barabarani ambao walifika eneo la tukio,wamekataa kuzungumzia tukio hilo wakidai
wao siyo wasemaji.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments