SERIKALI KUMALIZA KERO ZOTE ZA MAJI-WAZIRI MKUU-Septemba 21,2017
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini zikiwemo wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.