WAKAZI KATAVI WALALAMIKIA KUKITHIRI KWA TAKA KATIKA MAKAZI YAO-Septemba 21,2017
WAKAZI wa kata ya Mpanda Hotel
Manispaa ya Mpanda wamelalamikia uwepo wa taka katika makazi yao kwa muda mrefu
hali inayosababisha kuhofia magonjwa ya mlipuko.
Wamesema uchafu umerundikana
majumbani na barabarani kwa Zaidi ya wiki tatu bila kuzolewa licha ya kila
mwezi kuchanga pesa kwa ajili ya uzoaji taka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi
cha kuzoa taka katika Kata ya Mpanda Hotel Bw. Emmanuel Mgiuna amesema wanashindwa kuzoa taka kwa sababu hakuna gari
wala kizimba kwa ajili ya kukusanyia uchafu.
Afisa
mtendaji wa kata ya Mpanda Hotel Bw.Hamidu Sungura amekataa kuzungumzia tatizo
la mrundikano wa taka katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Mpanda Hotel kwa muda
mrefu huku naye Bibi Afya wa kata hiyo Bi.Grace Kunchela kwa sharti la
kutorekodiwa sauti akisema zoezi la kuzoa litaanza kesho.
Tatizo la
kukithiri kwa taka katika maeneo mbalimbali katika manispaa ya Mpanda kumetokea
kutokana na kutokuwepo kwa magari ya kutosha kwa ajili ya kauzoa taka pamoja na
vizimba vya kukusanyia taka.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com,Ukuasa
wa Facebook P5Tanzania Limited
Comments